Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Eto'o kujiuzulu Cameroon lafikia hapa

Samuel Etoo 1 Samuel Eto'o

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa kandanda Samuel Eto´o ambaye sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon, ameomba kujiuzulu wadhifa huo lakini uamuzi huo wa Eto´o umekataliwa na kamati yake ya kiutendaji ambayo imesema bado inamuamini.

Eto'o mwenye rekodi ya mchezaji bora wa Afrika mara nne  na ambaye ameshikilia wadhifa huo wa Rais wa shirikisho la Soka la Cameroon tangu Desemba 11 mwaka 2021, amekuwa akikabiliwa na tuhuma za mienendo isiyofaa, upangaji matokeo na rushwa.

Hatma ya Kocha wa Cameroon Rigobert Song iko pia matatani baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON inayoendelea huko Ivory Coast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live