Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Alaba na mashabiki wa Madrid lafikia pabaya

Alaba Messi Benzema Sakata la Alaba na mashabiki wa Madrid lafikia pabaya

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Real Madrid David Alaba alinyanyaswa kibaguzi baada ya kupiga kura yake kwa Lionel Messi na si Karim Benzema katika Tuzo za ubora za FIFA.

Pamoja na wachezaji wengine kuwachagua kwanza wachezaji wenzao, Alaba hakumtanguliza Benzema ambaye ni mchezaji mwenzake ndani ya Real Madrid.

Alaba alitoa pointi zake 5 kwa Messi, na kumuweka Benzema nafasi ya pili akifuatiwa na Mbappe nafasi ya tatu.

Mara baada ya zoezi hilo alama ya #AlabaOut ililianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikifuatiwa na maneno ya kibaguzi dhidi yake. Wapo walioweka emoji za nyani kwenye posti mbalimbali katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Kupitia mtandao wa Twitter Alaba aliamua kujieleza kwanini alimchagua Messi kwanza na kuweka wazi kuwa hii haimaanishi kuwa hamkubali Benzema, alisisitiza kuwa kwake Benzema anabaki kuwa mshambuliaji mahiri Duniani na hii haibadiliki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live