Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saka tajiri mtoto, wala haringi

Saka Dogo Saka tajiri mtoto, wala haringi

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hivi karibuni tovuti ya Capology, ilitoa orodha ya mastaa wa England wenye utajiri mkubwa walioitwa timu ya taifa na mmoja wao ni Bukayo Saka ambaye hadi kufikia sasa anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 10 milioni.

Saka amewekeza pia kwenye biashara zinazomwingizia pesa na anatajwa atatajirika zaidi kutokana na soka na mambo mengine. Hata hivyo unajua anapigaje pesa.

ZINAKOTOKA PESA

Saka anapata pesa kutoka ndani na nje ya uwanja. Kwanza ni kupitia mshahara wake ambao unafikia Pauni 295,000 kwa wiki.

Pia ana biashara ya pilipili aliyoizindua katika siku za hivi karibuni ambayo inatarajiwa kumpa zaidi ya Pauni 2 milioni kwa mwaka.

Anapiga pesa za kutosha pia kupitia kampuni mbalimbali anazofanya nazo kazi. Kampuni ya kwanza ni New Balance ambayo inamlipa kwa kuvaa viatu vyao. Taarifa zinaeleza analipwa zaidi ya Pauni 1 milioni kwa mwaka kutokana na dili hilo.

Pia ana mikataba ya kuwa balozi na Kampuni za Amazon Prime, Fiverr, Beats na Call of Duty ambazo zote kwa pamoja zinampa zaidi ya Pauni 5 milioni kwa mwaka.

NDINGA Ferrari 458 Spider Mercedes Benz GLC-Class Audi A8 Audi Q7 Range Rover

MSAADA KWA JAMII

Tangu mwaka 2022, Saka amekuwa akitoa pesa kuchangia taasisi ya Bigshoe inayojihusisha na kusaidia matibabu ya watoto kutoka nchi mbalimbali duniani. Pia inaelezwa huchangia gharama za upasuaji kwa watoto 120 huko Kano, Nigeria.

NYUMBA

Alitumia Pauni 2.3 milioni kununua nyumba London, England mwaka 2019 ambayo ndani yake ina eneo kubwa analolitumia kufanya mazoezi pale anapokuwa kwenye mapumziko.

Kwenye nyumba hiyo aliyoinunua akiwa anatimiza umri wa miaka 18, pia anaishi na wazazi wake.

BATA NA MAHUSIANO

Kwa sasa yupo kwenye mahusiano na Tolami Benson ambaye amekuwa naye tangu mwaka 2020 na walikuwa wakifanya siri hadi siku za hivi karibuni na wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali.

Tolami anafanya kazi za mitindo na analipwa kwa kuwa modo wa kampuni mbalimbali. Saka ni mmoja kati ya mastaa ambao hawapendi sana bata na muda wa mapumziko huwa anautumia kucheza game akiwa mwenyewe ama na ndugu zake.

Chanzo: Mwanaspoti