Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saka kulamba Mkataba mpya Arsenal

Bukayo Saka New Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal wanapanga kuwaongezea mkataba wachezaji wake kadhaa mikataba wakiongozwa na Bukayo Saka,Gabriel Martinelli, pamoja na William Saliba.

Arsenal wana mpango wa kuwaongezea mikataba wachezaji hao ambao wanaonekana wanaweza kuifanya klabu hiyo kua bora siki za mbeleni, Kwasababu kwenye orodha ya wachezaji hao wote vijana wadogo wenye vipaji vikubwa.

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu wa klabu hiyo Edu raia wa Brazil ndio anasimamia utaratibu mzima wa kuhakikisha vijana hao wanaongezewa mikataba kwajili ya kuimarisha timu na kuirudisha kwenye ubora wake uliozoeleka.

“Tunahitaji kutoa motisha kwa wachezaji wetu ambao wana mustakabali mzuri na klabu yetu” Tunataka kufanya vitu kwenye njia sahihi, na kupanga vitu bora zaidi”Alisema Edu.

Arsenal ambao wanaonekana kua na msimumzuri mpaka sasa chini ya kocha Mikel Arteta ambapo mpaka sasa klabu hiyo inaongoza ligi kuu ya Uingereza ikiwa imeshinda nmichezo saba kati ya nane waliyocheza kwenye ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live