Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saka azua hofu Arsenal

Arsenals English Midfielder Bukayo Saka 771764881 Bukayo Saka akiugulia majeraha

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka alishindwa kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Nottingham Forest wikiendi iliyopita baada ya kuumia kifundo cha mguu akimpa presha kocha Gareth Southagate kuelekea fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza mwezi huu.

Saka aliumia dakika ya 15 tu ya mchezo huo baada ya kugongana na mchezaji wa Nottingham Forest, Lenad Lodi huku zikiwa zimebaki wiki tatu kabla ya fainali za Kombe la Dunia kuanza nchini Qatar.

Baada ya mchezaji huyo kuumia alijikaza na kuendelea kucheza. Hata hivyo katika dakika ya 27 winga huyo alishindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Reiss Nelson ambaye katika mechi hiyo alicheka na nyavu mara mbili.

Baada ya kuumia katika mchezo huo kocha wa England, Gareth Southagate amepata hofu juu ya hali ya winga huyo ambaye anategemea kumjumuisha kikosini.

Endapo jeraha la Sako litakuwa kubwa kocha huyo atalazimika kusaka mchezaji mwingine atakayeziba pengo hilo jambo ambalo litamfanya atumie mwingi kusaka mbadala.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema anaamini Saka atakuwa nje baada ya kugongwa vibaya kwenye kifundo chake cha mguu.

“Sifahamu chochote kuhusu hilo. Tusubiri kuona siku zitakazofuata. Saka aligongwa mara kwa mara hakucheza kwa raha,” alisema Arteta.

Licha ya mchezaji huyo kuumia Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 ikizidi kupaa kieleleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England ikichuana vikali na Manchester City ambayo ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City wikiendi iliyopita.

Mabao ya Arsenal yaliwekwa kimiani na Gabriel Martinelli katika dakika ya tano ya mchezo huo na mawili yakifungwa na Reiss Nelson kwenye dakika ya 49 na 52, Thomas Partey dakika ya 57 pamoja na Martin Odrgaard aliyepachika msumari wa mwisho dakika ya 78.

Ikumbukwe kuwa England itakuwa bila nyota wake Reece James aliyeumia huku Kyle Walker akisiliziwa endapo atakuwa fiti baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live