Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saka aiumiza kichwa Arsenal

Bukayo Saka New Season Saka aiumiza kichwa Arsenal

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Arsenal imeingiwa na hofu baada ya Bukayo Saka kuumia katika mechi ya Ligi Kuu England kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bournemouth.

Naye kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate amepata mashaka kwani ameshataja majina ya kikosi chake kuelekea mechi zao za kimnataifa dhidi ya Australia na Italia.

Sasa kocha Mikel Arteta anaomba winga wake kuwa fiti kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Lens kabla ya kumenyana na Manchester City wikiendi ijayo.

Saka alikosa mechi ya Kombe la Ligi dhidi ya Brentford baada ya kuumizwa mguuni wakati wa mechi dhidi ya Tottenham Hotspur na hakuweza kufanya mazoezi kwa ajili ya mechi dhidi ya Bournemouth.

Saka alionekana ana maumivu makali baada ya kugongwa na beki wa Bournemouth Milos Kerkez dakika ya 75.

Baadaye akafanyiwa mabadiliko nafasi yake akichukua Fabio Vieira na alifanyiwa uchunguzi na madaktari wa Arsenal kufahamu ukubwa wa jeraha hilo.

Baada ya mechi kumalizika kocha Mikel Arteta alisema: "Nadhani aliguswa mguuni sikupata nafasi ya kuzungumza naye. Gabriel Jesus alipata majeraha pia. Tutaendelea kuwafuatilia hali zao halafu tutaona. Nafikiria kuhusu vipi nitaiandaa timu dhidi ya Lens na Man City."

Saka, 22, alifunga dhidi ya Bournmouth licha ya kutolewa kutokana na majeraha, Martin Odegaard alicheka na nyavu pia kupitia mkwaju wa penalti, huku Kai Havertz na Ben White wakiimaliza mchezo dakika za lala salama.

Chanzo: Mwanaspoti