Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saka, Martinelli waihakikishia Arsenal alama tatu

Bukayo Saka Arsenal Newcastle United 1tmfir5wqddm15br90b540r71 Bukayo Saka akishangilia baada ya kuifungia Arsenal goli la ufunguzi

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bukayo Saka and Gabriel Martinelli walikuwa katika kiwango bora kabisa na kuizamisha New Castle united kwa magoli 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Arsenal walishuhudia mbio zao za kucheza michezo nane mfululizo EPL pasipo kupoteza zikizimwa na Liverpool wikiendi iliyopita.

New Castle ambayo kwa mara ya kwanza imecheza mbele ya Kocha wao Eddie Howe wanabaki kuwa Timu pekee EPL kucheza michezo 12(kabla ya huu wa leo) pasipo kushinda hata mchezo mmoja.

Magoli ya Arsenal katika mchezo huo uliopigwa Emirate syamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 56 ya mchezo na G. Martinelli dakika ya 66 ya mchezo.

Kwa ushindi huo Arsenal imepanda mpaka nafasi ya tano katika msimamo wa EPL ikiwa na alama zake 23, huku New Castle ikiendelea kuburuza mkia wakiwa na alama sita pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live