Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saka, Kane watakata England ikiichapa Ukraine

Bukayo Saka Vs Harry Kane Wafungaji wa magoli ya England

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

England imeendelea kuvuna alama kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Ukraine katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Euro 2024 uliopigwa katika uwanja wa Wembley Leo Jumapili.

Mabao ya England ya kocha Gareth Southgate yamefungwa na Harry Kane ambaye alimalizia mpira wa krosi safi ya Bukayo Saka nyota wa Arsenal ambaye alikuwa kwenye ubora mkubwa kwenye mchezo huo.

Saka kisha akafunga bao la pili kwa Three Lions akitumia pasi ya kiungo mkabaji wa Liverpool Jordan Henderson mabao yote mawili yakifungwa ungwe ya kwanza.

Kwa matokeo hayo, England wamekuwa na ushindi wa asilimia 100 kwenye mechi mbili za kwanza kwenye kuwania nafasi ya kushiriki mashindano ya Euro ambayo yatakuwa muhimu kwa vijana wengi wa kikosi hicho kwani wanatazamiwa kuwa watakuwa wamikomaa kiakili kuyakabili mashindano akiwemo Saka mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live