Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sajili zilizovunja benki Ulaya msimu huu

Caicedo Chelseaaaaaa Sajili zilizovunja benki Ulaya

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku zimepita ambapo mikataba ya uhamisho yenye thamani ya euro milioni 100 ilikuwa adimu. Sasa ni jambo la kawaida, haswa linapokuja suala la wanasoka bora ambao bado wana miaka mingi iliyobaki kucheza.

Soko la uhamisho limeongezeka na imekuwa kawaida kwa timu kudai fedha nyingi kwa wachezaji wao wakuu. Mikataba kadhaa ya uhamisho iliyothibitishwa na kuripotiwa msimu huu wa majira ya joto ni uthibitisho wa hili.

Msimu huu wa majira ya joto, tumeona ongezeko kubwa la mikataba ya fedha nyingi. Huku kukiwa bado na muda mwingi kwenye dirisha la uhamisho wa wachezaji, bado tunaweza kuona klabu nyingi zikivunja benki ili kupata huduma za wachezaji zinazowatamani.

Makala haya yameangalia ada tano za uhamisho zilizoripotiwa kutoka kwenye dirisha hili la uhamisho ambazo ni za juu zaidi...

#5 Malcom - Euro Milioni 60

Al-Hilal ni moja ya Klabu ya Saudi Aarabia ambayo imeonesha nia kubwa katika soko la usajili msimu huu wa majira ya joto. Wamewasajili wachezaji kama Kalidou Koulibaly, Sergej Milinkovic-Savic, Ruben Neves na Malcom katika miezi michache iliyopita.

Malcon amegharimu euro milioni 60. Kusema ukweli, winga huyo wa Brazil alikuwa na kampeni nzuri sana ya 2022-23 kule Zenit St. Petersburg. Alifunga mabao 26 na kutoa pasi tisa za mabao kwenye mechi 33 katika mashindano yote.

Lakini tofauti na wachezaji wengine mashuhuri ambao wamehamia Al-Hilal muhula huu, Malcom hakuwa akichezea kwenye klabu ambayo ipo kwenye Ligi Kuu tano bora za Ulaya.

#4 Kai Havertz – Euro Milioni 75

Chelsea ilimsajili Kai Havertz kutoka Bayer Leverkusen msimu wa majira ya joto wa 2020 kwa kitita cha euro milioni 80. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alikuwa na matukio machache ya kukumbukwa akiwa na jezi ya Chelsea.

Hata hivyo, hakuwahi kufikia kilele kilichotarajiwa kwake katika kipindi cha misimu mitatu aliyocheza Stamford Bridge. Makubaliano kati ya mashabiki na wachambuzi yanaonekana kuwa hakuweza kuhalalisha bei yake wakati akiwa klabuni hapo.

Kwa ujumla, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alifunga mabao 32 na kutoa asisti 15 katika mechi 139 kwenye michuano yote aliyoichezea Chelsea. Lakini licha ya kutokuwa na msimu mzuri kule Stamford Bridge, 'The Blues' waliweza kurejesha karibu kiasi chote walicholipa kupata kwa huduma yake miaka mitatu nyuma.

Yeye si mshambuliaji wa kati na tayari wana wachezaji wazuri wa kati wa kushambulia kwenye malipo yao.

#3 Rasmus Hojlund – Euro Milioni 75

Ni kweli kwamba Manchester United ilihitaji kuwekeza kwa mshambuliaji mchanga wa kati ambaye anaweza kuwa kwenye jezi hiyo kwa muda mrefu. Lakini licha ya kipaji kikubwa alichotoa katika msimu wa 2022-23, Rasmus Hojlund ni mchezaji ambaye bado hajathibitishwa na kuna uhakika mdogo wa kufanikiwa Old Trafford.

Alifunga mabao tisa pekee na kutoa pasi nne za mabao katika mechi 32 za Serie A msimu uliopita. Kutoa kiasi cha euro milioni 75 kwa mchezaji kunaweza kuwa kama mchezo wa kubahatisha.

#2 Lucas Paqueta – Euro Milioni 81

Lucas Paqueta alijiunga na West Ham United kutoka Lyon kwa dili la euro milioni 42 msimu uliopita. Alifunga mabao matano na kutoa asisti saba katika mechi 41 katika mashindano yote kwa 'Wagonga Nyundo' hao msimu uliopita. Ana miaka miwili zaidi katika mkataba wake wa sasa na West Ham na hawana nia ya kumuuza hivi sasa.

Manchester City waliripotiwa kuweka mezani dau la euro milioni 81 kwa ajili ya kiungo huyo wa kati wa Brazil wiki iliyopita. Ingawa yeye ni mchezaji bora, akiwa na Euro milioni 81, Paqueta bila shaka ni ghali zaidi.

Lakini hata kiasi hicho kikubwa huenda kisiipate City, mchezaji huyo kwani West Ham wameripotiwa kukataa ombi lao na wanataka zaidi.

Wakati City hawana uhaba wa fedha za kulipa, wanapaswa kuwa waangalifu na historia wanayoweka kwa kuvunja benki ili kusajili mchezaji ambaye anaweza asiboresha sana timu yao.

#1 Moises Caicedo - Euro milioni 133

Moises Caicedo ameripotiwa kukataa nafasi ya kwenda Liverpool baada ya 'Wekundu' hao kukubaliana ada na Brighton & Hove Albion kwa huduma yake siku chache zilizopita. Kiungo huyo mchanga amejiunga na Chelsea ambayo ilikuwa ikimwania kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Sky Sports, Chelsea wamelipa kitita cha euro milioni 133 kumnunua kiungo huyo wa Ecuador. Caicedo bila shaka ni mmoja wa viungo bora zaidi wa ulinzi kwenye Ligi Kuu England na ameweka historia ya usajili ghali zaidi katika historia ya ligi hiyo.

Hicho ni kiasi cha fedha cha kuchukiza kutumia kwa kiungo mkabaji. Ili kuweka mambo sawa, wachezaji kama Declan Rice na Rodri wote wana thamani ya euro milioni 90.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: