Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sajili za hovyo Barani Ulaya

Paul Pogba A 1536x864 Paul Pogba

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati huu klabu kubwa Barani Ulaya zikipambana kunasa saini za mastaa wapya, tena kwa pesa ndefu ni mahali gani watapigwa za kichwa kama ilivyowahi kutokea huko na kuhesabika kama usajili wa hovyo kabisa kuwahi kufanyika?

Usajili wa beki Harry Maguire kutoka Leicester City kwenda Man United kwa ada ya Pauni 80 milioni mwaka 2019, ulipigiwa kura na kuchaguliwa kuwa uhamisho wa hovyo zaidi kuwahi kutokea kwenye soka.

Uhamisho wa Paul Pogba kurudi Man United akitokea Juventus kwa ada ya Pauni 89.3 milioni mwaka 2016 ulitajwa kushika namba mbili, wakati ule wa Liverpool walipomnasa Andy Carrol kutoka Newcastle United kwa Pauni 35 milioni mwaka 2011 umeshika namba tatu kwenye kura za usajili wa hovyo kwenye soka.

Usajili mwingine wa hovyo ni ule wa Ali Dia alipojiunga na Southampton mwaka 1996 baada ya mtu mmoja kudai ni mchezaji bora wa dunia wa zamani, George Weah, hivyo Kocha Graeme Souness alishawishika na kumsajili.

Usajili wa Eden Hazard wa Pauni 150 milioni kwenda Real Madrid mwaka 2019 na ule wa Chelsea ilipolipa Pauni 15 milioni kumsajili Adrian Mutu mwaka 2003 ambaye baadaye ilimwondoa baada ya kufeli kwenye vipimo vya matumizi ya dawa zinazopigwa marufuku michezoni, nao pia wamo kwenye orodha.

Fernando Torres kwenda Chelsea, Angel di Maria kwenda Man United na Joey Barton kwenda Rangers nao umeingia kwenye 10 bora ya usajili wa hovyo kuwahi kutokea kwenye mchezo wa soka, huku kukiwa na dili nyingine zilizofanikiwa, lakini iliyoshika namba moja ni ile ya Erling Haaland kwenda kujiunga na Manchester City kwa ada ya Pauni 51.2 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live