Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saini ghali za makocha Ulaya

Xabi Alonso X Pep G Saini ghali za makocha Ulaya

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool italazimika kulipa pesa nyingi sana kama fidia ya kupata huduma ya kocha Xabi Alonso inayomsaka atue Anfield kwenda kuchukua mikoba ya Jurgen Klopp mwisho wa msimu huu.

Kutokana na kocha Alonso kuwa na kibarua cha kuinoa Bayer Leverkusen ambapo mkataba wake utafika tamati majira ya kiangazi 2026, ambapo miamba hiyo ya Bundesliga inahitaji ilipwe Pauni 20 milioni.

Kwa sasa, Bayern Munich ndiyo timu iliyolipa pesa nyingi kuvunja mkataba wa kocha, ilipolipa Euro 25 milioni kumng'oa, Julian Nagelsmann kutoka RB Leipzig mwaka 2021.

Kutokana na hilo, hizi hapa dili za makocha ambao mikataba yao ilivunjwa kwa pesa nyingi kama fidia ili kuhamia kwenye timu nyingine.

10.Maurizio Sarri - Pauni 5milioni

Napoli kwenda Chelsea, Julai 2018

Chelsea ilitoa Pauni 5 milioni kunasa huduma ya kocha Maurizio Sarri ilipomnasa kutoka Napoli. Kwa sasa kocha huyo anainoa Lazio baada ya kupita kwa muda huko Juventus.

9.Ronald Koeman - Pauni 5milioni

Southampton kwenda Everton, Juni 2016

Goodison Park imeshuhudia majina wenye majina makubwa kwa miaka ya karibuni wakifanya kazi hapo. Mdachi huyo alitua Everton akitokea Southampton, lakini alidumu miezi 18 tu Goodison Park akafukuzwa.

8.Brendan Rodgers - Pauni 5milioni

Swansea kwenda Liverpool, Juni 2012

Liverpool ililipa Pauni 5 milioni kunasa huduma ya Rodgers kutoka Swansea City mwaka 2012. Na hakika kocha huyo alikuja kufanya mambo Anfield, ambapo ilibaki kidogo tu anyakue ubingwa wa Ligi Kuu.

7.Jose Mourinho - Pauni 5.2milioni

Porto kwenda Chelsea, Juni 2004

Mourinho aligharimu pesa nyingi Chelsea wakati wanavunja mkataba wake huko FC Porto mwaka 2014. Tajiri, Roman Abramovich alitambua umuhimu wa kuwa na huduma ya kocha huyo huko Stamford Bridge.

6.Jose Mourinho - Pauni 6.9milioni

Inter kwenda Real Madrid, Mei 2010

Baada ya kuipa mataji matatu Inter Milan ndani ya msimu mmoja, Real Madrid ilivutiwa na huduma ya kocha Jose Mourinho na kwenda kuvunja mkataba wake, ikilipa pesa nyingi, Pauni 6.9 milioni.

5.Ruben Amorim - Pauni 8.6milioni

Braga kwenda Sporting Lisbon, Machi 2020

Jina jingine linalohusishwa na kwenda kurithi mikoba ya Klopp huko Anfield. Kocha Amorim kwa sasa anatamba Sporting, ambao walilipa Pauni 8.6 milioni kuvunja mkataba wake huko Braga mwaka 2020.

4.Brendan Rodgers - Pauni 8.8milioni

Celtic kwenda Leicester, Februari 2019

Baada ya kuondoka Liverpool na kurudi zake Celtic, kocha Rodgers alionyesha kiwango bora na kuwavutia Leicester City waliokwenda kumchukua na kuvunja mkataba wake kwa Pauni 8.8 milioni.

3.Andre Villas-Boas - Pauni 13.3milioni

Porto kwenda Chelsea, Juni 2011

Mreno huyo aliwasili London Magharibi akiwa mwenye jina kubwa kutokana na kile alichofanya FC Porto, ambacho kiliwashawishi Chelsea kulipa Pauni 13.3 milioni kuvunja mkataba wake huko Ureno.

2. Graham Potter - Pauni 21.5milioni

Brighton kwenda Chelsea, Septemba 2022

Brighton ilikusanya mkwanja wa maana kupitia kocha wake Graham Potter baada ya Chelsea kuvutiwa na huduma yake akapige mzigo Stamford Bridge. The Blues ililipa Pauni 21.5 milioni.

1. Julian Nagelsmann - Pauni 21.7milioni

RB Leipzig kwenda Bayern Munich, Aprili 2021

Bayern Munich ililipa ada ya Euro 25 milioni sawa na Pauni 21.7 milioni kuvunja mkataba wa kocha Nagelsmann huko RB Leipzig ili akapige mzigo Allianz Arena. Hiyo ni fidia kubwa zaidi kwenye soka.

Chanzo: Mwanaspoti