Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido kwa vitu vyake, bado yupo sana

Saido Ntibazonkiza Ant Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibazonkiza

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ mwishoni mwa msimu ulioisha jina lake lilianza kutajwa miongoni mwa watakaopitiwa na panga, lakini mchezaji huyo ameonekana kupindua meza mbele ya kocha wake, Nasreddine Nabi na sasa ni nguzo muhimu ya mauaji kikosini.

Yanga iliinasa saini ya Saido kwa mkataba wa miaka miwili kupitia usajili wa dirisha dogo Oktoba 2020 muda mfupi akitokea kuifunga Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki akiwa na timu yake ya taifa ya Burundi.

Alianza maisha Jangwani kwa kishindo akihusika katika mabao sita kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara, akifunga mawili dhidi ya Dodoma Jiji na Prisons na kutoa asisti nne, mbili katika mechi waliyoshinda 3-0 dhidi ya KMC na asisti nyingine moja kila mechi waliposhinda 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji, walipoichapa Ihefu mabao 3-1.

Hata hivyo, baadaye majeraha ya muda mrefu yalimsumbua huku matatizo ya kinidhamu ikiwamo kutaka kutoka uwanjani baada ya kufunga bao wakati mechi ikiendelea kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa akipingana na uamuzi wa aliyekuwa kocha wa wakati huo Juma Mwambusi wa kumuanzishia benchini, vikaanza kumfuta Saido katika ramani za Yanga.

Lakini baada ya kuomba radhi kwa tukio hilo ambalo lilishuhudiwa ‘live’ na kocha Nabi ambaye alikuwa jukwaani siku hiyo baada ya kuwasili kupewa ajira Yanga, Saido sasa amekuwa mtu mpya. Amerejeshwa kikosini baada ya kuumia kwa Yacouba Songne na anakiwasha ile mbaya. Msimu huu tayari amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili.

Straika wa zamani wa timu hiyo, Said Bahanunzi alisema Saido alifunga mabao mawili timu ikiwa na uhitaji na presha kubwa na kwamba ni fundi wa mbinu na kucheza kwa akili. “Angekuwa mchezaji muoga angekosa, lakini alijivika ujasiri akapiga,” alisema.

Mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar, George Kavila alisema uzoefu wa straika huyo ni faida kwa timu yake hasa wakati wa mechi ngumu za kupata matokeo.

Chanzo: Mwanaspoti