Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido kama kawaida Burundi

Saido Burundi Kiungo wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza aitwa Timu ya Taifa ya Burundi

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Simba, Saido Ntibazonkiza ni miongoni mwa nyota 27 walioitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Burundi kitakachocheza mechi mbili nyumbani baadaye mwezi huu katika mashindano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika, Marekani, Canada na Mexico.

Ntibazonkiza ni miongoni mwa wachezaji wachache wakongwe walioitwa na kocha Etienne Ndayiragije kwa ajili ya kibarua hicho walichonacho wengine wakiwa ni beki Nsabiyumva Frederic anayeichezea Vasteras SK ya Sweden na Nahimana Shassiri anayeitumikia Bandari ya Kenya.

Kocha Ndayiragije mbali na Ntibazonkiza pia amewaita kikosini kipa Nahimana Jonathan wa Namungo na Justin Ndikumana wa Coastal Union hivyo kufanya wachezaji wanaocheza hapa Tanzania kuwemo katika kikosi hicho kuwa watatu.

Matumaini makubwa kwa kikosi cha Burundi kwenye mechi hizo mbili yapo kwa kiungo anayefanya vizuri hivi sasa katika kikosi cha OGC Nice ya Ufaransa, Ndayishimiye Youssouf.

Kikosi hicho cha Burundi kinaundwa na makipa Rukundo Onesime, Ndikumana na Nahimana wakati mabeki ni Eric Ndizeye, Nsabiyumva, Weymans Marco, Mikombozi Derrick na Nduwarugira Christopher.

Viungo ni Aruna Madjaliwa, Bigirimana Abeid, Irutingabo Tresor, Emmanuel Mvuyekure, Shassir Nahimana, Ntibazonkiza, Aaron Musore, Mussa Omar, Youssouf Ndayishimiye na Jospin Nshimirimana.

Washambuliaji ni Fiston Abdulrazak, Shaban Hussein, Pacifique Niyongabire, Kilongozi Richard, Sudi Abdallah, Donasiyano Irakoze, Jean Claude Girumugisha, Bienvenu na Liongola Jordi.

Chanzo: Mwanaspoti