Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido awatumia ujumbe mzito Horoya

Saidoo Simba Saido awatumia ujumbe mzito Horoya

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ amefunguka kuwa kwa namna yoyote itakavyokuwa lazima wachukue alama tatu za Horoya AC kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wikiendi hii.

Saido alisema, wataingia uwanjani wakiwa na malengo ya aina moja pekee ambayo ni kuwafunga Horoya na kwa bahati mbaya kwa Horoya na nzuri kwao ni ari na morali waliyonayo kwa sasa.

Akizungumza nasi, Saido alisema, ushindi wa mabao 3-0 waliyopata mbele ya Mtibwa Sugar umewaongezea nguvu zaidi na kwamba kilichobaki kwa sasa ni kwenda kuvuna alama tatu mbele ya Horoya.

“Nafikiri kwa sasa namna ambavyo tulivyo tupo na morali kubwa sana kuelekea kwenye mechi yetu ya tarehe 18 dhidi ya Horoya. Tunahitaji alama tatu kwenye mechi hiyo.

“Ushindi wa mabao 3-0 dhidi Mtibwa Sugar umetuongezea nguvu zaidi na hiyo ni faraja kwetu na mashabiki wawe tayari kwa kufurahia,” alisema.

Machi 18, Simba watamenyana na Horoya kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao kimsingi watakuwa wanahitaji alama tatu ili kuweka hai matumaini yao ya kwenda robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live