Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido ataka rekodi yake Yanga

Saido Rekodi.jpeg Saido bado hajafanikiwa kupachika bao akiwa na Geita Gold

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Geita Gold, Said Ntibazonkiza 'Saido' amesema anapambana katika kikosi hicho ili kuifikia au kuivunja rekodi yake ya mabao saba na assisti tatu aliyoiweka akiwa na waajiri wake wa zamani timu ya Yanga.

Saido ambaye bado hajacheka na nyavu hadi sasa alisema bado ana muda wa kufanya makubwa akiwa na timu yake hiyo mpya kama jinsi ambavyo alifanikiwa akiwa na Yanga hivyo atapambana kwa hali na mali ili kutoa kilicho bora.

"Kwa sasa ni mapema sana kwa sababu mbio hizi bado ni ndefu na ushindani nao umeongezeka, kikubwa kwangu ni kuiwezesha timu yangu ifanye vizuri hivyo suala la kufunga litakuja na sina wasiwasi," alisema na kuongeza;

"Mafanikio ya timu yanaletwa na umoja, ushirikiano wetu hivyo sitaki kuweka ahadi ya kusema nitafunga sana au laah! japo matumaini yangu ni kuona naifikia rekodi niliyoiweka Yanga au kuivunja," alisema staa huyo wa Burundi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa timu hiyo, Leonard Bugomola alisema tangu nyota huyo ametua nchini kumekuwa na manufaa makubwa kwenye kikosi chao kwani uzoefu wake anautumia vizuri kuwafundisha vijana wadogo wenye ndoto za kufanikiwa.

"Timu yetu ina vijana wadogo sana hivyo unapokuwa na mchezaji kama Saido kwenye kikosi anasaidia mambo mengi kwa sababu ni mzoefu na uwepo wake unaongeza morali kwa vijana kupambana zaidi ili kufika alipo," alisema.

Mabao saba aliyofunga na assisti tatu alizochangia ni kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara tu aliyocheza katika mechi 18 kati ya 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live