Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido asicheze mechi ya AlAhly - Shabiki Simba

Saido Amtetea Bocco Mashabiki Kumzomea Saido asicheze mechi ya AlAhly - Shabiki Simba

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindaki wa klabu ya Simba, Mzee Mwenda amesema kuwa ili timu yake ishinde mchezo dhidi ya Al Ahly basi kocha asimpange kucheza Saido Ntibazonkiza kwani amekuwa mchoyo wa kutoa pasi kwa wenzake hivyo kuwanyima nafasi za ushindi timu hiyo.

Mwenda ameongeza kuwa, Simba haina washambuliaji kwa sasa hivyo kocha anapaswa kuanzisha mabeki wengi na viungo wengi ili kuukamata mchezo huo wa robo fainali ya CAFCl ambao unatarajiwa kupigwa Ijumaa, machi 29, 2024.

“Ningependa Saido akae nje aanze Onana kwa sababu Saido ni mchoyo hataki kutoa pasi. Kama kocha anataka ushindi kwenye mechi hiyo, achezeshe beki wawili wa kulia na mabeki wawili wa kushoto, kiungo acheze Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma aende kiungo cha juu na Kanoute angekuwepo na yeye angemweka wakawa viungo watatu.

“Tunapunguza washambuliaji kwa sababu hatuna washambuliaji, kina Jobe sio washambuliaji ni wachezaji ambao hata kwenye Ndondo Cup nikipewa timu siwezi kuwapanga. Wametuletea kajanjajanja ili wapate thumuni.

“Huwezi kumsifia Jobe wala Fredy, hawamo. Kyombo anawazidi, Bocco anawazidi lakini wameenda kutuletea Simba. Simba ni kubwa na kuwa watu wanaishusha hadhi Simba,” amesema Mzee Mwenda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live