Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido amtetea Bocco kuzomewa na mashabiki

Saido Amtetea Bocco Mashabiki Kumzomea Saido amtetea Bocco kuzomewa na mashabiki

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Saidi Ntibanzokiza 'Saido' amesema mashabiki wao wanapaswa kuwa na uvumilivu kwani siku hazifanani, kuna wakati unaweza kukutana na ugumu na wakati mwingine uraisi.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya Power Dynamos, Saido alisema, anawashukuru mashabiki wa Simba kwa kuendelea kuwa nao pamoja kila wakati lakini akawasihi waendelee kufanya hivyo hata kwenye kipindi kigumu.

"Utaona mchezo wa leo ulikuwa mgumu lakini hata hivyo sisi wachezaji tulipambana kuhakikisha tunapata matokeo. Mashabiki nao pia wanatakiwa kutuelewa kuna nyakati mechi inakuwa ngumu kama hivi leo, kikubwa tumevuzu lakini mliona wakati Bocco anaingia mashabiki walikuwa wanamzomea lakini ndio huyo aliyetufanya tupate goli," alisema Saido.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live