Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido alikuwa hataki kubaki Simba

Saido 38834065 Saido alikuwa hataki kubaki Simba

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia TV3, Wakanda Republic amedai kuwa aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza hakutamani kuendelea kusalia Simba.

Wakanda amesema hayo baada ya Saido kupewa mkono wa heri na klabu ya Simba baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

"Kama ungemuuliza Saido kama anatamani kuendelea kuwa Simba, jibu lake nina uhakika lingekuwa ni hapana. Kwa sababu mara nyingi amekuwa akipewa shutuma na mashabiki wa Simba.

"Shutuma ambazo zimekuwa zikienda moja kwa moja kwake kwamba si mchezaji ambaye wana simba wanaamini atawavusha, kwahiyo hata kwake yeye nina uhakika ule moyo wa kuichezea Simba haukuwepo tena," amesema Wakanda Republic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live