Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido akiri umaarufu una gharama

Saido 1 Goal Saido akiri umaarufu una gharama

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo fundi wa mpira wa Simba, Saido Ntibazonkiza, amekiri wakati mwingine umaarufu huwa ni kama kero pale mashabiki wanapoingilia faragha zao, japo amesema ni changamoto ambazo kama mchezaji analazimika kuzioea kwa vile anahitaji sapoti ya watu hao katika maisha ya soka.

Kauli ya Saido imekuja baada ya juzi kuvamiwa na shabiki alipotimba kwenye Uwanja wa Uhuru kushuhudia chama lake la zamani la Geita Gold, likivaana na KMC na kutoka na ushindi wa mabao 2-0, ambapo licha ya kujichanganya na watu ili asijulikane mashabiki walibaini na kumvaa alipokuwa akitoka uwanjani hapo.

Akiwa hana hili wala lile, ghafla saido alijikuta akivamiwa na shabiki huyo aliyekuwa na nia ya kutaka kumkumbatia, huku Mwanaspoti likishuhudia, lakini staa huyo akawahi kumzuia akitaka kwanza ajitambulishe.

Shabiki huyo aliyekuwa akiongea lugha za Kiswahili na Kilingala alipiga magoti, huku akimuomba msaada wa pesa na katika kuepusha mambo mengi, Saido alitoa noti ya Sh 5,000 na kumpa licha ya kuombwa Sh 2,000.

Baada ya kupewa pesa hiyo, shabiki huyo aliyeonekana kama aliyelewa aliendelea kumng'ang'ania akitaka kumkumbatia Saido, mara apige magoti kama vile anataka kumsujudia, ghafla akaanza kumwambia amuombee, lakini staa huyo alimzuia. Saido alipoona anaendelea kung'ang'aniwa na shabiki huyo alikubali kupiga naye picha na wakati wanapata picha ya pamoja (shabiki huyo) alipata mpenyo wa kumwambia ya moyoni kuhusu soka.

"Napenda mnavyocheza watatu hasa pasi ianzie kwa Chama, uipokee wewe na kisha uitoe kwa Baleke fundi wa kucheka na nyavu, mkipangwa wote nakuwa na amani ya kupata matokeo ya ushindi," alisema shabiki huyo aliyejitambulisha na mnazi mkubwa wa Simba.

Mara baada ya kupata sekeseke hilo, Saido aliliambia Mwanaspoti, "Naheshimu wanaotusapoti kwenye kazi zetu, ila kuna wakati zinatokea changamoto mbalimbali, ndio maana unaweza ukawakuta wachezaji wana kofia hadi usoni wanapotokea maeneo kama haya, kwani umaarufu ni gharama."

Saido pia aliweka bayana namna alivyofurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo ya zamani ya Geita aliyoichezwa kabla ya kutua Simba katika dirisha dogo la msimu huu na kukiri ilistahili ushindi iliyopata.

"Nimekuja kuwasapoti, wanacheza vizuri, wana wachezaji wanajituma kwa kadri wawezavyo ndio maana wamepata ushindi ugenini,"alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live