Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido aipania Yanga CCM Kirumba

Saidoooooo Geita Saido aipania Yanga CCM Kirumba

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Godfather wa Bunjumura kiungo wa soka ambaye alipata umaarufu mkubwa akiwa na Klabu ya Yanga, Saido Ntibazonkiza, amefunguka kuwa mechi yao ijayo dhidi ya Yanga, kwake anaitazama kwa umakini mkubwa.

Saido ambaye alifunga bao moja na kutoa pasi ya bao kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting juzi Jumatano, alisema kila mechi kwake atakuwa anaicheza kama fainali na hata kwenye mchezo wao ujao na Yanga atacheza kwa hali ileile.

Akizungumzia mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Saido alisema: “Kwangu kila mchezo naucheza kama fainali. Siyo mimi tu, bali kila mchezaji kwenye timu yetu anacheza kwa moyo huo.

“Ndiyo, Yanga ni timu kubwa na siwezi kusema neno lingine tofauti na kwenda kujituma zaidi na kuweza kuisaidia timu yangu kupata alama tatu muhimu. Hayo ndiyo malengo yangu pamoja na timu.”

Saido aliondoka kwa mazingira yasiyotarajiwa na wengi mwishoni mwa msimu uliopita kwa madai ya awali ya kuwa ni mtovu wa nidhamu na kisha baadaye ikaja taarifa kuwa ameondoka kwenye klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live