Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saidi Ntibanzokiza 'Saido' amegomea mkataba wa mwaka mmoja, huku akiutaka Uongozi wa Simba SC kumpa mkataba wa miaka miwili.
Saido ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao imebakisha miezi sita ya kuendelea kubakia Simba SC, ambayo imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao msimu buu, ambao wamepanga kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Kiungo huyo alijiunga na Simba SC wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita, akitokea Geita Gold ambako alisaini mkataba wa miezi sita kabla ya kutua Msimbazi.
Zipo baadhi ya timu zinatajwa kuwania saini ya kiungo huyo, ambaye msimu uliopita alitwaa Ufungaji Bora akipachika mabao 17, sawa na aliyekuwa Mshambuliaji wa Young Africans aliye Misri kwa sasa sasa, Fiston Mayele. Kati ya hizo APR ya nchini Rwanda ndiyo imeonekana kuonyesha nia kubwa.