Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza, amesema anamshukuru Mungu kwa timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania na kwamba hilo ndio muhimu kwanza, kupata kiatu cha ufungaji bora ni ziada.
Saido amesema, kwenye mchezo huo uliopigwa Juni 6, 2023 kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, kama wachezaji walikuwa na mpango mmoja tu wa kuibuka na ushindi na si kwamba walitaka yeye afunge magoli matano kati ya hayo sita kama ilivyotokea.
"Kwangu mimi Simba kwanza mambo ya kiatu cha ufungaji bora yakitokea huko mbele nitamshukuru Mwenyezi Mungu. Tulijipanga kucheza ili tushinde lakini wachezaji wenzangu kweli walipoona nimepata magoli kama matatu wakawa wananitengenezea kweli nafasi za kushinda zaidi," alisema Saido.