Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido Ntibazonkiza kuendeleza moto kwa Dodoma Jiji leo?

Saido 1 Goal Saido Ntibazonkiza

Sun, 22 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usajili mpya ndani ya klabu ya Simba kwenye dirisha dogo la mwezi Januari Saidoo Ntibazonkiza inawezekana akaendeleza moto wake katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji leo.

Mchezaji Saidoo Ntibazonkiza amekua kwenye kiwango bora tangu ajiunga na wekundu hao hao wa msimbazi akitokea klabu ya Geita Gold.

Kiungo huyo fundi amecheza michezo miwili ya ligi kuu ya NBC ndani ya timu hiyo na yote akifanikiwa kuhusika kwenye mabao.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Yanga ameshafanikiwa kufunga mabao matano kwenye michezo miwili ya ligi kuu ya NBC akiwa na klabu ya Simba, Ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa na watu wengi kwani watu wengi walitazamia kama ni usajili ambao uongozi wa klabu ya Simba uliukurupukia.

Mchezaji Saidoo Ntibazonkiza mpaka sasa amehusika kwenye mabao saba katika klabu ya Simba ndani ya michezo miwili akifunga matano na kupiga pasi mbili za mabao, Swali kubwa ni je kuendeleza ambacho amekifanya katika michezo miwili iliyopita? Hakuna mwenye majibu zaidi ya mchezaji mwenyewe.

Mchezaji huyo alijiunga na klabu ya Simba baada ya kua na kiwango bora sana ndani ya klabu ya Geita Gold na kuwavutia wekundu wa Msimbazi kuiwinda saini yake kwa udi na uvumba, Na mchezaji huyo tangu amejiunga na Simba amejaribu kuwaonesh viongozi wa klabu hiyo hawakukosea kumsajili kutokana na ubora wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live