Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido, Mukoko Waapa Kuimaliza Simba kwa Mkapa

Saidoo Saido, Mukoko Waapa Kuimaliza Simba kwa Mkapa

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MASTAA wawili wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ na Mkongomani, Mukoko Tonombe, wamejiapiza kwa mashabiki kwamba watapambana kwa kadiri ya uwezo wao kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo wao unaofuata dhidi ya Simba.

Watani hawa Simba na Yanga watakutana Desemba 11 huku Simba akimkaribisha mtani wake, Yanga kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara. Kwenye mchezo uliopita walipoku–tana, Yanga iliwafunga Simba 1-0 kwenye Ngao ya Jamii.

Saido alisema: “Ki–kubwa ni kuomba uzima na afya kwa Mungu, kwa sababu nimejiandaa vizuri kuhakikisha yule Saido wa zamani ambaye mashabiki wa walimmisi anarudi na kasi mpya.

“Na huu ni mwanzo tu wa ligi, hivyo nitaendelea kufunga sana mabao mengi pale nitakapokuwa napata nafasi, kwa hiyo mashabiki wetu watarajie mambo mazuri kutoka kwetu.”

Kwa upande wake Mukoko, alisema: “Mechi na Simba ni ngumu na tutapambana sana kuweza kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo huo ili kuwapa furaha mashabiki zetu kama mchezo uliopita tulipokutana na mtani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live