Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido Milioni Moja Kila Mechi Yanga

Saidoo Saido Milioni Moja Kila Mechi Yanga

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

IMEFAHAMIKA kuwa mshambuliaji mkongwe, raia wa Burundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’, anaingiza Sh milioni moja katika kila mchezo atakaoucheza akiwa akiwa amevaa jezi namba 60 Yanga kwenye mashindano yote na mechi za kirafiki.

Kiungo huyo tangu ametua hapo, amefanikiwa kubeba mataji mawili, lile la Kombe la Mapinduzi, mwaka jana na Ngao ya Jamii msimu huu.

Mrundi huyo ameonekana kurejea kwa kasi kubwa katika msimu huu kutokana na kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza chini ya Mtunisia, Nasreddine Nabi.

kiungo huyo anapata kiasi hicho kwa makubaliano waliyokubaliana katika mkataba wake huo ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kabla ya kusaini mkataba huo katika msimu uliopita, aliomba apewe jezi namba 10 aliyomkuta anaivaa Yacouba Songne lakini Mburkinabe huyo alikataa, ikabidi Mrundi akubali kuvaa namba 60 baada ya kutangaziwa dau.

Alisema kuwa Yacouba aligoma kuiachia jezi hiyo kabla ya viongozi kumbembeleza na kushikilia msimamo wake wa kutoiachia namba hiyo 10 anayoendelea kuivaa.

Aliongeza kuwa baada ya Yacouba kuendelea kugoma, wadhamini wa timu hiyo, GSM walimshawishi kumuahidi kumpa kiasi hicho cha fedha kila atakapocheza mechi akiwa amevalia jezi hiyo namba 60 na ndipo Saido akakubali.

“Wengi walikuwa hawafa­hamu kili­chokuwa kinaen­delea juu ya jezi namba 10 ambayo anaivaa Yacouba, ilizua utata mkubwa kutokana na Saido kuitaka ambayo alikuwa anaivaa tangu akiwa anacheza Ulaya na nyumbani kwao Burundi.

“Saido mwenyewe alikuwa tayari kumpa Yacouba dola 10, 000 (zaidi ya Sh 2OMil) ili amuachie jezi hiyo namba 10, lakini alizikataa na kushikilia msimamo wake.

“Jezi hiyo namba 60 anayoivaa Saido imeonekana kumnufaisha, kwani katika makubaliano yake na viongozi ambayo yapo katika mkataba, wamekubaliana kumlipa shilingi milioni moja katika kila mchezo atakaoucheza kuanzia alipojiunga na Yanga hadi hivi sasa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Yanga kwa kupitia Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela, hivi karibuni alisema: “Mkataba ni siri kati ya mchezaji na uongozi, hivyo ngumu kuweka wazi kila kitu kilichopo katika mkataba.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live