Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido, Mayele wapeleka lawama kwa mwamuzi

HERERIMANA HARUNA Kocha Mbeya kwanza, Hererimana amshushia lawama mwamuzi wa mchezo

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza FC Haruna Hererimana amemuangushia lawama Mwamuzi wa mchezo uliowakutanisha dhidi ya Young Africans, uliochezwa jana Jumanne (Novemba 30), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Mwamuzi hance Mabena alipewa mamlaka na kamati ya waamuzi, TFF na Bodi ya Ligi Kuu ‘TPLB’ kuchezesha mchezo huo uliomalizika kwa Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kocha Hererimana amesema Mwamuzi alishindwa kutenda haki kwenye mchezo huo, kwani hakuweza kusimamia sawa sawa sheria 17 za soka.

Amesema alifanya kusudi kuibeba Young Africans ili ishinde mchezo huo, jambo ambalo anaamini sio sawa hasa ikizingatiwa klabu hiyo ya Dar es salaam ni kubwa na ina uwezo wa kushindwa bila usaidizi wa Mwamuzi.

“Kama timu ni kubwa ishinde kwa uwezo wake na sio kusaidiwa na marefa, Yanga ni klabu ambayo inaweza kufanya lolote ndani ya dakika 90, lakini isiwe kwa msaada wa jambo lolote.”

“Tuache mpira uchezwe kwa kutumia sheria 17 za mchezo wa soka, tusizipindishe ili kuinufaisha timu fulani iweze kushinda.” amesema Kocha huyo kutoka nchini Burundi

Katika hatua nyingine Kocha Hererimana amewalaumu Wachezaji wake kwa kukosa umakini hasa katika kipindi cha kwanza cha mchezo, ambapo timu yake iliruhusu kufungwa mabao mawili.

“Wachezaji wangu walikosa umakini, kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri na hatua hiyo iliwafanya wapinzani wetu kutuadhibu kwa mabao mawili.” ameongeza Kocha Hererimana.

Ushindi wa Young Africans dhidi ya Mbeya Kwanza FC unaendelea kuiweka kileleni klabu hiyo ya Jijini Dar es salaam kwa kufikisha alama 19, na rasmi inaanza maandalizi ya mchezo wa mzunguuko wanane dhidi ya Simba SC, utakaochezwa Desemba 11, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live