Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido: Kuwa sehemu isiyo sahihi ni adhabu

Saido Two Goals.jpeg Saido Ntibanzokiza

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Kimataifa wa Burundi ambaye anakipiga katika kikosi cha Simba Sc Saido Ntibazonkiza ameshare ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Saido amekuwa akisemwa vibaya na mashabiki wa Simba kuwa kiwango chake kimeshuka na hana mchango tena kwenye klabu hiyo huku kukiwa na taarifa kuwa huenda akaachana na timu hiyo mwisho wa msimu huu.

"Mtu mkubwa haadhibiwi kwa kuchapwa fimbo bali adhabu ya mtu mzima ni kuwa sehemu isio sahihi kwake na hakika nimejifunza," amesema Saido Ntibazonkiza.

Inaelezwa kuwa, uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuachana na Saido Ntibazonkiza atakapomaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu 23/24 lakini Kocha Abdelhak Benchikha anamuhitaji Kuelekea msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live