Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido, Chama wampa kiburi Robertinho

Chama Saido Mlk Saido, Chama wampa kiburi Robertinho

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ametamba ubora wa safu yake ya ushambuliaji ni chanzo kikubwa kwao kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba Februari 11, wanatarajiwa kuanza mchezo wao wa kwanza wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa ugenini nchini Guinea kukabiriana na Horoya.

Mbrazil huyo alisema: “Timu yetu imejawa na wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa haswa wakijaliwa vipaji vya maana, tunaamini timu hii ina uwezo wa kushindana vyema haswa kimataifa.

“Kama utaona timu kubwa nyingine kama TP Mazembe na nyingine utaona ni timu ambazo zimezungukwa na wachezaji wenye vipaji ndio maana hufanya vizuri pia.

“Tunao kina Clatous Chama, Pape Sakho ,Mzamiru Yassin, Saido na wengine wengi ndani ya Simba. Ni wachezaji bora na wenye vipaji vikubwa jambo ambalo ni msingi mzuri kwetu kwenda kupambana katika michuano ya kimataifa,” alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live