Kiungo wa Simba SC anayecheza Mtibwa Sugar kwa mkopo Said Khamis Ndemla, ameomba radhi kwa kitendo cha kinyama alichomfanyia Kiungo Sadio Kanoute, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana Alhamis (Juni 23), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Ndemla alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi sehemu ya paja Kanoute, aliyekua kwenye harakati za kuokoa mpira uliokuwa unaelekea langoni mwa Simba SC.
Kiungo huyo mzawa ametumia muda wake kuandika ujumbe wa kuomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambao umeonesha anajutia kosa alilolifanya.
“…Ninafahamu sana kwamba kujutia nilichofanya na kuomba msamaha hakutabadilisha au kufuta kusimamishwa, lakini ni vyema kujua jinsi ya kujifunza kutokana na makosa yako … ningependa kuchukua nafasi hii kuwasilisha msamaha wangu wa dhati kutoka moyoni mwangu kwa kaka yangu Sadio Kanoute, timu ya Simba na mashabiki!
Aidha, napenda kuwaomba radhi wachezaji wenzangu na mashabiki wa soka kwa ujumla. Siwezi kuficha kiwango ambacho nimewakatisha tamaa. Nisameheni sana"
Soma hapa chini post ya Ndemla;