Said Benrahma amekuwa mchezaji wa kwanza wa Westham United kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa michuano ya Ulaya tokea mwaka 1980 Davis Cross aifunge Real Madrid Castilla kwenye kombe la European Cup Winners.
Benrahma ameifikia rekodi hiyo baada ya kufunga mabao hayo kwenye sare ya Westham 2-2 KRC Genk kwenye mchezo wa mzunguko wanne wa michuano ya UEFA Europa Ligi uliochezwa usiku wa kuamkia leo nchini Ubelgiji.
Mabao hayo ya Benrahma yameibeba westham na kuendelea kuwa kinara wa kundi H kwa kuwa na alama 10 hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kufuzu kwenda hatua ya mtoano ya 32 bora ya michuano hiyo.