Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safu nzuri ya Ulinzi inakupa uhakika wa kushinda mataji? njoo tubishane

Mugalu, Mkude ,Kapombe Wachezaji wa Simba Mugalu (alieachwa mwanzo wa msimu), Mkude na Kapombe

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nasubiri mtu aniambie ule msemo maarufu wa Alex Ferguson halafu tubishane. Ule msemo kwamba "Safu nzuri ya ushambuliaji itakushindia mechi, halafu safu nzuri ya ulinzi itakushindia mataji". Nitabishana sana.

Huu msemo haukuwa kweli kwa Simba iliyotisha misimu minne mfululizo. Ni kweli ile Simba ilikuwa na safu nzuri ya ulinzi lakini ilijengwa zaidi katikati kuja mbele.

Msimu mmoja walikuwa na James Kotei 'Iron man' katika kiungo cha chini akicheza sambamba na Jonas Mkude. Halafu mbele yake walikuwa na Clatous Chama. Katika benchi walikuwa na Mzamir, Hassan Dilunga pamoja Haruna Niyonzima! Hiyo ni safu ya kiungo tu

Mbele walikuwa na Emanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco. Hapo nje walikuwa na Shiza Kichuya bora sana, na bwana mdogo Rashid Juma angeweza kuingia na kukupa kitu kama siku ile dhidi ya As Vita pale Lupaso.

Alipoondoka Emmanuel Okwi tayari aliingia Miquissone kuziba nafasi yake. Badala Kotei aliingia Fraga na baada ya Fraga aliingia Taddeo Lwanga. Wote hawa waliitendea haki safu ya kiungo na ushambuliaji ya Simba.

Ile Simba ilitengenezwa zaidi kuanzia katikati kuja mbele. Kama unabisha angalia waliokuwa 'back up' ya mabeki. Paul Bukaba asingekupa nusu ya Erasto Nyoni hata Juuko asingekupa Sergie Wawa.

Ila katikati kuja mbele angetoka mtu na kuingia mtu. Niyonzima angecheza vema kwa Chama. Hata Dilunga amewahi kuamua mechi Chama akiwa benchi. Unamkumbuka Mzamir kwenye eneo la Jonas Mkude dhidi ya As Vita pale taifa?

Ni kweli "A good defensive line will win you titles" lakini siyo kwa Simba ile. Ile Simba iliundwa zaidi katikati kuja mbele.

Ni kama ambavyo naamini Yanga hii imetengenezwa zaidi katikati kuliko maeneo mengine. Tazama 'back up' katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ya Yanga halafu tazama kiungo chao.

Khalid Aucho, Yanick Bangala na Zawadi Mauya kama mido za chini. Mudathir Yahya, Sureboy, Feisal Salum na Aziz Ki mbele yao. Wakati mwingine Farid na BM33 wanasogezwa eneo hilo. Ni utajiri wa kiasi gani wanao Yanga katika midfield??

Ni kweli "Defense wins you titles" lakini sio kila mara. Nipo pale njoo tubishane

Chanzo: www.tanzaniaweb.live