Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari yetu bado ndefu kushinda makombe - Ten Hag

Erik Ten Hag Manchester United 2022 23 Kocha wa Manchester United Erik ten Hag

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: eatv.tv

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amesema kikosi chake bado kipo kwenye hatua za awali kwenda kwenye mafanikio na bado wanasafari ndefu hivyo wanapaswa kuwa bora kila siku ili kufikia malengo.

"Naelewa mashabiki wanandoto kubwa, Lakini tuko mwanzoni mwa mchakato na bado tuko mbali. Tunapaswa kuendelea kuamini kimtazamo na fikra. Tunapaswa kuweka malengo ya juu kila siku. Lazima tuwe bora zaidi kama tunataka kushinda mataji.’’ Amesema Erik ten Hag

Kocha huyo amesema hayao baada ya kikosi chake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Arsenal na huu ni ushindi wao wa 4 mfululizo kwenye ligi kuu England EPL ikiwa ni kwa mara ya kwanza wanafanya hivyo tangu April 2021.

Kikosi hicho kimefikisha alama 12 kipo nafasi ya 5 ikiwa ni tofauti ya alama 3 dhidi ya Arsenal ambao ndio vinara wakiwa na alama 15 kwenye msimamowa EPL.

Chanzo: eatv.tv