Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya mwisho ya Kocha Mumba

Mumba4876 Safari ya mwisho ya Kocha Mumba

Sat, 2 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali nchini wakiongozwa na msemaji mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligarambwike, jana wamejitokeza kwa wingi kumzika Mkufunzi wa Makocha Tanzania Marehemu Ahmed Mumba.

Marehemu Mumba ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Makocha Mkoa wa Morogoro’TAFCA’ amefariki dunia Jumamosi iliyopita hospital ya Mloganzira Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa jana Makaburi ya Kolla Mkoani Morogoro.

Mara baada ya Kocha Mumba kufariki Mwili wake ulirejea nyumbani kwake Kihonda Mbuyuni Kata ya Mafisa ambapo wadau mbali mbali wa soka wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma wamefulika nyumbani kwa marehemu kushiriki lbada ya kumuombea iliyoongozwa na Mashehe zaidi ya 7.

Wingi wa Mashehe hao unatokana na Marehemu Mumba enzi za uhai wake kuwa jirani na Mwenyezi Mungu kwa kushiriki swala 5 kwenye misikiti mbali mbali ya Mkoa wa Morogoro.

Baadhi ya Mashehe hao ni pamoja na Shehe Koba wa Msikiti wa I.G.P Mstaafu Alhaj Omar ldd Mahita ulipo Mafiga, Shehe Ally Omar wa Msikiti Mkuu wa Morogoro ulipo Boma Road.

Wengine ni Shehe Shaban Juma wa Msikiti wa Awayya Uliopo Mawenzi ambaye ndiye aliyepiga Adhana swala ya saa 10 iliyofanyika nyumbani kwa marehemu akitanguliwa na swala ya kumuombea Marehemu yenye Takbira 4.

Enzi za uhai wake Marehemu Mumba akiwa katibu wa TAFCA huku mwenyekiti wake akiwa John Simkoko chama hicho kinatambuliwa na shirikisho cha Mpira wa Miguu Afrika’CAF’.

Hivyo Hayati Mumba na Simkoko mara kwa mara kupitia chama hicho walitoa mafunzo ya ukocha yanayotambuliwa na CAF,makocha kibao wakiwemo wa Simba,Yanga Azam wameshiriki mafunzo hayo na kukabidhiwa leseni zinazotambuliwa na CAF na Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Baadhi ya makocha hao ni pamoja na Seleman Matola, Simba Abibu Kondo Mtibwa Sugar Mecky Mexime Kagera Sugar, John Tamba, Polisi Tanzania,Zuberi Katwira Ihefu.

Wengine ni Juma Kaseja, Ulimboka Mwakingwe, Athuman Kairo Ally Jangalu.na Bi.Edina Lemma aliyekuwa kocha wa Yanga Princess Kama kawaida Mwandishi wa Mtandao huu alizunguka kona zote kwenye msiba huo akisaka picha za watu maarufu zicheki hapo chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live