Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Yanga yaota mbawa

Yanga Sc Media Officer Hassan Bumbuli Spge0rsmuoel148ictakf1pod?fit=1200%2C800&ssl=1 Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari ya Yanga kwenda kuweka Kambi Jijini Arusha kwa ajilli ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya KMC Oktoba 19 haitakuwepo tena.

Klabu ya Yanga ilipanga kwenda kuweka Kambi Arusha kama sehemu ya maandalizi dhidi ya mchezo wao na KMC.

Akizungumzia hatua hiyo , Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema;

"Tumekaa na benchi la ufundi tukashauriana tukaona haina haja tena ya kwenda kuweka kambi Jijini Arusha kwa kuwa tutawachosha wachezaji wetu na hasa wale waliopo katika majukumu ya timu zao za Taifa"

"Itawabidi wakifika hapa waunganishe tena ndege kwenda Arusha kuungana na timu, jambo ambalo tunaona tutawakosesha muda wa kupumzisha miili yao, na badala yake kambi itakuwa hapa hapa Dar, na watakaporudi watajiunga na wenzao kabla ya kusafiri Oktoba 17 kwenda Songea" amesema Bumbuli

KMC na Yanga zitacheza mechi Oktoba 19 katika uwanja wa Maji Maji Songea, huku KMC wakiwa na alama 1 wakati Yanga wana alama 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live