Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Yanga imeishia Robo Fainali - Jemedari

Jemedari Said The Voice Less VIDEO: Safari ya Yanga imeishia Robo Fainali - Jemedari

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Bongo, Jemedari Said amesema safari ya Yanga SC kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inaishia Robo Fainali na si vinginevyo.

Jemedari amesema, si Yanga tu hata Simba SC hawana uhakika wa kutoboa Nusu Fainali licha ya wapinzani wao Al Ahly kuonekana kupungua kiwango chao.

"Huwezi kuona sasa hivi Mamelodi anamfikiria Yanga kama ambavyo Yanga sasa hivi anamfikiria Mamelodi. Mamelodi yeye anajua akikutana na Yanga atamfunga basi lakini Yanga sasa hivi anawaza anajua anakutana na timu kubwa na ngumu.

"Ndio maana hata Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alipoulizwa maoni yake alisema timu anazoona zinaweza kufika fainali na kubeba ubingwa ni Mamelodi na Al Ahly, amesema hivyo na yeye ni Rais wa Yanga kwa nini asiitaje Yanga?

"Hakuitaja Yanga sababu anajua hana wachezaji wenye ubora wa kufanana na Mamelodi. Hata Simba, pamoja na kwamba wanakutana na Al Ahly ambayo kiwango kimeshuka lakini hata wao wanajua wanakutana na timu ngumu ambayo inaweza kuwatoa," alisema Jemedari.

View this post on Instagram

A post shared by Prisca kishamba (@officialpriscakishamba)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live