Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Stars CHAN yafika kikomo, wakubali kichapo cha magoli 3

Uganda Vx Stars .jpeg Stars imekubali kichapo cha magoli 3-0 nchini Uganda

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" sasa ni rasmi imetupwa nje katika kinyang'anyiro cha kuwania kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-0 kutoka kwa Uganda jioni hii.

Ushindi huo wa Uganda unawafanya kujihakikishia ushindi wa jumla wa magoli 4-0 baada ya mchezo wa awali uliopigwa Jijini Dar es Salaam Stars kukubali kichapo cha goli 1-0 kipigo kilichomuondoa Kocha Kim Poulsen.

Magoli ya Uganda katika mchezo wa leo yamefungwa na Moses Waisa kwa mkwaju wa penati, Basangwa (52) na Rodgers (75).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live