Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Singida United, Mbeya City kushuka daraja yashika kasi, Azam yapoteza dira

94639 Pic+azam Safari ya Singida United, Mbeya City kushuka daraja yashika kasi, Azam yapoteza dira

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jahazi la Singida United limezidi kuzama baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Biashara United, huku Azam ikipoteza nafasi ya kuisogelea Simba baada ya kulazimishwa sare 1-1 Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Uhuru.

Singida United ikicheza ugenini kwenye Uwanja wa Karume, Mara ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Biashara na kuzidi kujiweka katika mazingira magumu ya kubaki katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Singida United inayofundishwa na kocha Ramadhan Nswazurwimo inashikilia mkia katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 10, baada ya kucheza michezo 19 hadi sasa.

Shujaa wa Biashara United alikuwa mshambuliaji Innocent Edwin aliyefunga mabao mawili wakati bao la kufutia machozi Singida United likifungwa na Mtikila Hussein.

Dar es Salaam, Azam watajilaumu wenyewe kushindwa kulinda ushindi wao baada ya kuiruhusu Tanzania prisons kupata bao la kusawazisha katika dakika 90+5.

Prisons ilipata bao la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Jumanne Nimkaza goli ambalo liligomewa na wachezaji wa Azam wakidai mpira haujaingia golini, lakini picha za marudio za TV zilionyesha kipa Razack Abaloa aliokoa mpira huo ukiwa umevuka mstari wa goli.

Pia Soma

Advertisement
Azam ilitawala mchezo huo kwa sehemu kubwa ilikuwa ya kwanza kupata bao kuongoza katika dakika 45, lililofungwa na mshambuliaji Obrey Chirwa akiunganisha mpira wa krosi ya Bruce Kangwa.

Matokeo hayo yanaifanya Azam kubaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 38, na kupoteza nafasi ya kuisogelea Simba kileleni wenye pointi 50.

Katika michezo mingine Namungo ikiwa nyumbani Rungwa ilikubali kulazimishwa sare 1-1 na Alliance kwenye Uwanja wa Majaliwa.

Namungo ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Reliants Lusajo katika dakika 33, kabla ya Alliance kusawazisha kupitia Zabona Mayombya.

Ruvu Shooting imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Mtibwa Sugar kwa bao 1-0, shukrani kwa goli la Baraka Mtuwi alilofunga katika dakika 75.

Kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara wenyeji Ndanda wamefufuka na kuichakaza Mbao kwa mabao 3-0 na kujikwamua kutoka katika mstari wa kushuka daraja.

Mshambuliaji mkongwe Hussen Javu alifunga mabao mawili katika dakika 68, 88 na lile la mapema la Vitalisy Mayanga katika dakika ya 3, yametosha kuwapa Ndanda ushindi wa kwanza mnono nyumbani msimu huu.

Mbeya, safari ya Mbeya City kushuka daraja imeanza kushika kasi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa KMC kwenye Uwanja wa Samora, Iringa shukrani kwa bao la dakika 86 la Charles Ilamfia.

Mshambuliaji Yusuph Mhilu ameendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu baada ya kuiongoza Kagera Sugar kuichapa Mwadui kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Mhilu alifunga bao lake la nane msimu huu katika dakika 15, kabla ya mshambuliaji Kelvin Kongwe kufunga bao la pili dakika 38, huku la Mwadui ikipata bao la kufutia machozi kupitia Omary Nassoro katika dakika ya 46.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz