Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Marumo Gallants mpaka nusu fainali ya CAFCC

Marumo Gallants Er Marumo Gallants

Tue, 2 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hii ni safari ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambao ni wapinzani wa Yanga kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, hadi nusu fainali.

Gallants walifuzu kucheza michuano ya CAFCC baada ya klabu ya Mamelodi Sundowns kutwaa ligi kuu na michuano ya super 8 (FA), hivyo kikanuni ikabidi Gallants waende CAFCC kwa sababu walicheza fainali na Mamelodi licha ya kupoteza.

Licha ya kutofanya vizuri kwenye ligi kuu lakini klabu hii haitabiriki, inawachezaji wazuri japo upepo wa matokeo kwenye ligi umewakataa. Wanashika nafasi ya (14).

Pia, wanatumia vizuri uwanja wao wa nyumbani licha ya kutokuwa na mashabiki wengi.

Play off - CAFCC Al Ahli Tripoli 1 - 0 Gallants Gallants 3 - 0 Al Ahli Tripoli

Group stage - CAFCC Gallants 4 - 1 Al Akhdar Lupopo 1 - 2 Gallants USM Alger 2 - 0 Gallants Gallants 2 - 0 USM Alger Al Akhdar 4 - 1 Gallants Gallants 3 - 2 Lupopo

04 - Kushinda 02 - Kupoteza

Hawana tofauti kubwa na Yanga kwenye group stage, Yanga yeye alishinda (4) akasare (1) na akapoteza (1).

Quarter final - CAFCC Pyramids 1 - 1 Gallants Gallants 1 - 0 Pyramids

Semi final - CAFCC Yanga ? - ? Gallants.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live