Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Abraham mikononi mwa Mourinho

Image 407 1140x630.png Safari ya Abraham mikononi mwa Mourinho

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Chelsea, Aston Villa na Brentford zote zinadaiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kumsajili Mshambuliaji wa AS Roma, Tammy Abraham, ambaye mabosi wake wamepanga kumuuza katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa kocha Jose Mourinho ataondoka.

Inaelezwa kuwa Abraham mwenye umri wa miaka 26, alijiunga AS Roma kwa sababu ya Mourinho na ikiwa kocha huyo ataondoka basi hata yeye amepanga kuondoka kurudi England.

Chelsea inatajwa kuwa imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu kujua maendeleo yake na inamuona kama mchezaji sahihi wa kumsajili dirisha lijalo kwa sababu anafahamu vizuri mazingira ya Stanford Bridge.

Kwa upande wa Brentford wanataka kumsajili ili akazibe pengo la lvan Toney anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu ambapo timu nyingi kubwa zinamhitaji.

Aston Villa pia imekuwa ikimtamani kwa muda mrefu na wanawasi kwamba ifikapo dirisha lijalo la majira ya kiangazi Mshambuliaji Ollie Watkins huenda akatakiwa na timu kubwa hivyo Tammy anaweza kuwa mbadala.

Chanzo: Dar24