Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sadio Mane azindua uwanja aliojenga kijijini kwao

Mane  725178 Sadio Mane

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya jana ilikuwa siku kuwa sana kwa wananchi wa Bambali nchini Senegal ambapo mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane anayecheza klabu ya Al Nassr FC ya Saudi Arabia Sadio Mane alizindua uwanja alioujenga kwa gharama zake kijijini kwao Bambali. Uwanja huo ameupewa jina la Stade de Bambali.

Licha ya viongozi wengi wa Kiserikali kuhudhuria laikini pia wanakijiji walihudhuria pia kama sehemu ya uwanja huo, Uwanja huo umejengwa katika kijiji chake alichokiunda ambapo inaelezwa amejenga nyumba nyingi kwa ajili ya wanakijiji kuishi.

Ikumukwe kuwa mwaka 2022, Mane alionekana akicheza mchezo wa Kirafiki na Marafiki zake huko Kijijini kwao Bambali katika uwanja uliokuwa umejaa mchanga na mvua ilikuwa inyesha na kuonekana ameloa yeye na rafiki zake huku akiwa amechafuka kwa tope.

Inaelezwa hapo ndio wazo la Sadio Mane kujenga uwanja wake lilipokuja kwa leo la kutumiwa na wanakijiji lakini pia apate sehemu ya kucheza na marafiki zake pale anapoenda nyumbani kwa likizo.

Mpaka sasa Sadio Mane hajapost chochote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuonyesha uwanja wake, Mane na wenzake wamerudi Afrika kwa ajili ya kushiriki michuano ya AFCON inayotarajiwa kuanza Januari 13 nchini Ivory Coast.

Mchezaji/staa gani wa Tanzania uatamani kumuona akifanya mambo makubwa kama Sadio Mane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live