Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sadio Mane akiri mambo magumu Bayern

Sadio Mane X Lahm Sadio Mane

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Sadio Mane amekiri kuwa kuhamia kwake Bayern Munich hakujawa rahisi.

Nyota huyo kutokea Senegal alifanikiwa kufunga magoli manne katika mechi zake nne za mwanzo, baada ya hapo hali imekuwa ngumu.

Akizungumza na Uefa.com Mane ameeleza kuwa ”mambo yanaenda vyema, lakini kuhama klabu moja kwenda nyingine sio rahisi,"

"Nimekaa miaka nane mizuri sana nchini England, miaka sita Liverpool na miwili Southampton na sasa niko kwenye nchi mpya. Sio rahisi, kila kitu kimebadilika, watu, mazoezi, kila kitu,” amesema Mane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live