Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sadio Mane: Ninajivunia Senegal kutinga 16 bora

Krepin Diatta Mane Sadio Mane

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sadio Mane amewaambia wachezaji wenzake wa Timu ya Taifa ya Senegal kwamba anajivunia kwa kufanikiwa kutinga raundi ya 16 bora licha ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya England.

Nyota huyo anayekipiga Bayern Munich hajashiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Baada ya kipigo hicho Mane aliandika ujumbe wa pongezi kwa wachezaji wenzake kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya Senegal kung’olewa katika raundi ya 16 bora.

“Ndugu zangu ninajivunia safari yenu na mmelitetea taifa lenu kwa utu, mmeibeba nchi na watu wa Senegal kwa ujumla, tutasaka makombe mengine naamini, tutaendelea kujifunza na kla kheri kwa kila jambo,” alisema Mane.

Senegal ilipata pigo baada ya Mane kuumia kwani ndiye mchezaji tegemeo wa kikosi chao, staa huyo amefunga mabao 34 katika mechi 93 alizoichezea taifa lake.

Mane alikuwa na mchango mkubwa kwa taifa lake akilisadia kubeba ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mwaka huu. Vilevile amebeba tuzo kwa mara ya pili ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool ndiye aliyepiga penalti ya mwisho dhidi ya Misri kwenye fainali ya Afcon, Senegal ikiibuka na ubingwa baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 4-2. Fowadi huyo alifunga mabao manne kwenye michuano hiyo.

Ikumbukwe Mane alijumuishwa kikosini kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia, licha ya majeraha yaliyokuwa yakimsumbua baada ya kuumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya Bundesliga, Bayern Munich ilipomenyana na Werder Bremen mwezi uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live