Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sabilo afunguka ugumu Ligi Kuu

Sabilo Pic Sixtus Sabilo

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Mbeya City, Sixtus Sabilo mwenye mabao saba kwenye, amesema mshambuliaji yoyote kadri anavyofunga ndivyo anavyozidi kujiweka mtegoni mwa mabeki, hivyo jambo la msingi anaona ni kusaka mbinu mpya kila wakati.

Sabilo ambaye alianza vizuri msimu huu hajafunga kwenye mechi sita mfululizo, alilizungumzia hilo kwamba linampa chachu ya kuhakikisha haachwi mbali na mastraika waliofunga mabao mengi ambapo kinara wa mabao ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye 13.

“Ushindani unaanzia pale zinapokutana timu, lazima ndani ya timu wachezaji tunaangalia ni maeneo gani ya kuweka umakini zaidi, ndio maana inakuwa rahisi kunikaba kwani ndiye ninayeongoza kwa mabao ndani ya timu.

“Pia na mimi huwa naangalia aina ya ukabaji wa mabeki kila tunapokwenda kucheza dhidi ya wapinzani ambao wanakuwa mbele yetu kwa wakati huo, lengo ni kujua namna ya kupenya kwenda kuzitikisa nyavu za kipa wao, hivyo ni ushindani kwa kwenda mbele.”

Licha ya kukiri mzunguko wa pili ni mgumu zaidi, lakini aliapa atahakikisha anapambana kutupia mabao mengi na kwenda sawa wale ambao wapo juu yake.

“Ingawa wageni ndio wenye mabao mengi zaidi kama Mayele 13, Moses Phiri wa Simba 10, bado nina nafasi ya kupambana pia naamini wazawa tunaweza tukaendeleza pale aliishia George Mpole.”

Chanzo: Mwanaspoti