Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za TFF kusogeza mbele Tuzo za wachezaji hazina mashiko

Fei X Aziz Fainali Sababu za TFF kusogeza mbele Tuzo za wachezaji hazina mashiko

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimemsikiliza Anko wangu Karim Boimanda, Afisa Habari wa Bodi ya Ligi akielezea sababu za tuzo kusogezwa mbele, sababu zimezidi kuniacha na maswali mengi sana.

1- Wanasema sababu ni UBORA, yani wanataka tuzo ziwe bora TFF sasa cha kujiuliza hapa ni kuwa tukio za tuzo limekuja kama AJALI? Yaani tunaanza msimu na hatujaweka sawa suala la ubora kwa zaidi ya miezi tisa? Maana yake wametuambia wamefeli hapo Karume?

2- Mjomba wangu Boimanda wa TPLB anasema Kanuni ya 11 ni kuhusu tuzo za Ligi Kuu na sio tuzo za TFF, rudia vyema kusoma hapo yaani ni tuzo za TFF na sio za Ligi Kuu, sasa tunaomba msaada tunaombeni KANUNI ZA TUZO ZA TFF, zipo wapi? Maana Ligi Kuu zipo.

Tukae hapo kidogo, kumbe LIGI KUU kama Bidhaa haina TUZO za msimu, yaani inaweza kutoa tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi, Kocha bora wa mwezi ila tuzo za Ujumla HAWANA, kwahiyo ile Kanuni ya 11 kuhusu TUZO imewekwa kama geresha yani kisport tu.

3- TFF kuwa na tuzo zao ina maana kuwa wanaiuzia LIGI KUU (BODI YA LIGI) kuwa na tuzo zake binafsi? Na kama TFF inatoa tuzo za Ligi Kuu na Championship maana yake inaingiliana majukumu na BODI YA LIGI, maana yake chombo kimoja hakipo huru na kinamezwa na mwingine, tutavuka?

Duniani kote Shirikisho la soka kazi yake ni kusimama kama Mzazi kuhakikisha vyombo chini vinaendesha mambo yao, vinaipa uhuru wenye mipaka na vyenyewe vinajipa mamlaka yenye mipaka, kazi ya TFF ni kutunga sera, kusimamia sera na kuchakata maendeleo ya mpira sio kuzibana bidhaa mfano LIGI KUU.

4- Mjomba wangu Boimanda wa Bodi ya Ligi anasema sababu nyingine ni kuwa Ligi ya Wanawake haijaisha na pia kuna calendar ya FIFA ya mashindano, Anko kalenda ya FIFA inaanza TAREHE 03/06/2024 ndio maana Wachezaji wamechimba kwenda Indonesia wengi wao kwasababu mechi sio ya kalenda.

- Tuwasaidie tu kuwa duniani kote kwenye tuzo ambazo sio za kupiga kura WASHINDI woote ukiachana na MFUNGAJI BORA huwa wanafahamika kabla ya mechi ya mwisho ama muda mchache baada ya Ligi kutamatika, hivyo Kamati za tuzo maana yake zinaenda na UPEPO? Inafikirisha sana.

5- MWISHO kwakuwa mmetengeneza Kanuni kisha mmeivunja wenyewe, tuonesheni mfano wa KUWAJIBIKA kama ambavyo Klabu na Wachezaji mnavowawajibisha.

Kitaalam ni kuwa HAKUNA tuzo za msimu wa 2023/24 ila zitakuwepo tuzo za Msimu mpya wa 2024/25 ambapo tunaenda kuweka rekodi kama Taifa kuwa nchi ya kwanza duniani kugawa tuzo kabla ya msimu mpya kuisha.

Kwahiyo mijadala yoyote ya tuzo kwasasa ni batili na tutaitambua kama kusanyiko lisilo rasmi na halina kibali! Kwasababu Kiufundi mechi ya Ngao ya Jamii ni ufunguzi wa msimu mpya hivyo usiku wake ni tayari tupo msimu wa 2024/25.

Nadhani sasa ipo haja ya TASWA (Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo) kupambana kupata udhamini ili wawe na tuzo zao binafsi ili kuziba mashimo kama haya kama ilivyo duniani kote.

Na pia ni wasaa wa SPUTANZA (Chama cha Wanasoka) kupata udhamini mkubwa na kuacha kuishi kama Kamati ili nao wawe na tuzo zao kama ilivyo duniani kote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live