Mchambuzi wa soka Shafii Dauda amesema sababu za aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' zipo ila viongozi wamezificha.
Akichambua matokeo ya Simba kufungwa 5-1 na Yanga na kisha kumfulusha Robertinho, Shafii amesema;
“Mara nyingi naamini matokeo bora ya timu ni mchanganyiko wa uwajibikaji wa wahusika wote kuanzia bodi ,menejimenti ,benchi la ufundi ,wachezaji na wengine mfano mashabiki.
“Mfano kutoka kwa kiongozi wa juu kuja chini ukaangalia mfumo je upo sawa? Rais wa heshima ana mchango gani? Anakutana na bodi wakati gani? Bodi ifanye nini? Hivyo hivyo kuja chini hadi kwa watu walio nje.
“Juzi Rais wa heshima alisajili timu nyingine ya watu ambao ni nje ya timu. Uongozi ulioshinda na kuingia madarakani sidhani kama ulikuwa unapata sapoti.
“Ni vitu vingi ambavyo kwa jicho la kawaida havionekani lakini vina mchango mkubwa sana, football ni team game not an individual game ( mpira ni mchezo unaohusisha timu / umoja na sio mtu mmoja mmoja.
“Mkishinda mnashinda wote na mnafungwa wote mfano zoezi la kuvaa medali linakupa picha halisi ya kuona kuna wakina nani nyuma ya wachezaji kama timu.
“Mimi kama Dauda siamini kama Robertinho anatakiwa kufukuzwa, ukija head to head Robertinho na Yanga kashinda mechi moja, sare mechi moja na kafungwa mechi moja na hiyo sare bado alipata ubingwa (ngao)”
“Inawezekana kuna sababu zingine ambazo hawawezi kuzitaja, ndio maana taarifa inasema makubaliano ya pande mbili."