Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya Morrison kuachwa Simba hii hapa...

Bm Pic Data Sababu ya Morrison kuachwa Simba hii hapa...

Tue, 11 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MUDA mfupi kuanzia sasa kikosi cha Simba kitafika Afrika Kusini kutokea Tanzania huku wakiwa wamepitia nchini Kenya.

Simba wanakwenda nchini humo wakiwa na wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya mzunguko wa kwanza hatua ya robo fainali dhidi ya wapinzani wao Kaizer Chiefs.

Kikosi cha Simba kiliondoka nchini alfajiri ya leo Mei 11, 2021 huku wachezaji wanne wakishindwa kusafiri ikiwemo mshambuliaji, Bernard Morrison.

Uongozi wa Simba umesema sababu iliyomfanya Morrison kushindwa kusafiri ni taratibu za hati ya kusafiria (visa), kwani raia kutoka Ghana anatakiwa kuingia Afrika Kusini akiwa na visa.

Morrison yupo katika hatua za mwisho kukamilisha upatikanaji wa visa na huenda leo au kesho (Jumatano), akaanza safari ya kuungana na wenzake Afrika Kusini.

Wachezaji wengine walioachwa ni Said Ndemla, Miraji Athumani na Perfect Chikwende ambaye hana kibali cha kucheza mashindano hayo Ligi ya mabingwa Afrika.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu anasema hawezi kueleza kila sababu iliyofanya wachezaji hao kubaki hapa nchini ila Morrison atajiunga na wenzake.

Rweyemamu amesema Morrison kuna mambo ya kusafiria anayamalizia na wataungana nae katika kambi yao Afrika Kusini.

“Siwezi kueleza sababu ambazo Ndemla, Miraji zimewabakusha nchini ila Chikwende hana kibali cha kucheza mashindano Haya,” anasema Rweyemamu na kuongezea;

“Hali na morali ya wachezaji ipo vizuri kwani kuna kundi la kwanza ambalo limetangulia kwenda kuweka mazingira sawa ikiwemo, kuwepokea, timu itakapofikia pamoja na mambo mengine ya msingi.

“Kikubwa tunawaheshimu wapinzani wetu Kaizer kwani mpaka wamefika katika hatua hii si timu ya kuibeza lakini tunakwenda kupambana na ili kupata matokeo mazuri,”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz