Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya Gamondi kumchomoa Musonda ghafla kwenye kikosi

Gamondi Musonda Mede Sababu ya Gamondi kumchomoa Musonda kwenye kikosi

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa licha ya kumpanga mshambuliaji wake kennedy Musonda kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons, kocha huyo alilazimika kumchomoa kabla ya mchezo huo kuanza kutokana na kupata ugonjwa wa red eyes.

Musonda alikuwa kwenye 'line up' ya wachezaji waliopaswa kuanza kwenye mchezo huo lakini baada ya kupata ugonjwa huo, nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Farid Mussa.

“Ni kweli nilimpanga Kennedy Musonda aanze kwenye mchezo wa leo na alikuwa tayari kwa ajili ya mechi, ila baadae ikagundulika amepata tatizo la Macho (Red Eyes) ambayo ilimpelekea kupanda kwa homa.

“Sikuwa na namna nyingine zaidi ya kufanya mabadiliko ya haraka na kumpa nafasi Farid Mussa ambaye pia ametusaidia kwenye ushindi wetu wa leo“ amesema Miguel Gamondi.

Hata hivyo, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika Dimba la Sokoine Mbeya na kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC wakiwa na alama 40 katika michezo 15 waliocheza na kumaliza raundi ya kwanza ya ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live