Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu Mkude kuikosa Kaizer Chiefs yaanikwa

101680 Mkude+pic Sababu Mkude kuikosa Kaizer Chiefs yaanikwa

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA MKUU wa Simba, Didier Gomes amesema jambo kubwa analofurahia katika kikosi chake ni kutokuwa na majeruhi yeyote mpaka sasa.

Gomes amesema wana kibarua kigumu katika mchezo wao wa kesho, hivyo kutokuwa na majeruhi ni faida mojawapo katika kikosi chake.

“Mpaka leo asubuhi namaliza mazoezi hatukuwa na majeruhi yeyote, wachezaji wapo katika hali nzuri na wote wameonyesha hali ya kuhitaji kucheza mchezo huu.”

Gomes amesema katika mchezo huo atakayekosekana ni kiungo Jonas Mkude ambaye ana matatizo ya kifamilia.

“Wachezaji wote wapo vizuri na mazoezini wameonyesha kila mmoja anahitaji nafasi, Mkude hayupo ana matatizo.”

Simba na Kaizer Chiefs zitashuka dimbani kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo utakaochezwa saa 11:00 jioni.

Simba wanahitaji ushindi wa 5-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz