Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#SHIRIKISHOAFRIKA: Hiki hapa kikosi cha Yanga kinachoanza vs Marumo Gallants

Yanga Sauziiiiiiiii Wachezaji wa Kikosi cha Yanga

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya CAF na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Timu ya Yanga wanashuka Dimbani Royal Bafokeng muda mchache kutoka sasa kutupa karata yao dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika ya Kusini katika mchezo wa Nusu Fainali ya Mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakiwa hawana preaha baada ya Juma lililopita kutangaza Ubingwa wa Ligi uliokuwa ukifukuziwa kwa karibu na watani zao wa jadi Simba SC.

Mbali na Ubingwa, Yanga wanaingia katika mchezo huo wakiwa na uongozi wa mabao 2-0, ushindi walioupata katika Nusu Fainali ya mkondo wa kwanza mcheO uliopigwa katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na rekodi waliyonayo wenyeji Marumo Gallants wanapokuwa nyumbani katika Michuano ya Kombe la Shirikisho.

Hiki hapa kikosi cha Yanga kinachoanza mchezo wa leo;

D Diarra

Kibwana Shomari

Dickson Job

Ibrahim Bacca

Bakari Mwamnyeto

Yanick Bangala

Khalid Aucho

Mudathir Yahya

Kennedy Musonda

Tuisila Kisinda

Fiston Mayele

Chanzo: www.tanzaniaweb.live