Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#SHIRIKISHOAFRIKA: Hiki hapa Kikosi cha Yanga kinachoanza vs TP Mazembe

Yanga Kikosi.jpeg Kikosi cha Yanga kinachoanza vs TP Mazembe

Sun, 2 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Timu ya Yanga inashuka Dimbani muda mchache katika Uwanja wa Stade Mazembe mjini Lubumbashi.

Mchezo huo ni wa kukamilisha hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika huku wakiwa tayari washajikatia tiketi ya kusonga hatua ya Robo Fainali kundi D.

Katika mchezo wa leo Yanga inawakosa baadhi ya nyota wake muhimu akiwemo mlinda mlango Djigui Diarra na kiungo Khalid Aucho ambao wanatumikia adhabu ya kadi za njano.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakitafuta nafasi ya kuongoza kundi D mbele ya US Monastir kutoka Tunisia ambao nao pia wamefuzu huku TP Mazembe na Real Bamako wakiaga michuano hiyo.

Kikosi cha YANGA kinachoanza dhidi ya TP Mazembe

Metacha Job Lomalisa Bacca Mwamnyeto Bangala Mudathir SureBoy Moloko Musonda Mayele

Chanzo: www.tanzaniaweb.live